Taifa limeshapata suluhu Kinachofata ni mipango Na majaliwa Ya mwenyezi Mungu Analolipanga Mungu Huwezi kulipangua Alitupa Magufuli Kisha kamchukua Ametuachia jahazi Na sisi ndio abiria Jukumu letu ni kuchapa kazi Maana yupo wakusimamia Tutumbulie majambazi Wala rushwa maharamia Wasiotaka kufanyakazi Wapenda pesa zakuvizia Mama tuvushe Taifa zima lina imani nawe Mama tuvushe Hayati JPM Alikutuwa wewe Samia tuvushe Taifa zima Tunakutazama wewe Tuvushe Refarii ndio kabadilika Lakini uwanja ni ule ule Kazi juu ya kazi Tena mpenda haki Mtu wa mungu Fitina hataki Wala majungu Na ndoto za wanawake Shupavu zimetimia Na huyu ndio rais Wakwanza mwanamke Hapa Tanzania Mama Samia Tunakwenda kumalizia Miradi iliyobakia Pole yenu mnaohofia Aah, mama waonyeshe Unavyotekeleza Busisi bridge Na surrender Madaraja yote Mama waonyeshe Ooh, waonyeshe Unavyotekeleza Na flyover zilizobakia Mama waonyeshe Ooh, waonyeshe Unavyotekeleza Standard gauge Air Tanzania Mama waonyeshe Ooh, waonyeshe Unavyotekeleza Barabara, Elimu bure pia Mama waonyeshe Oh, waonyeshe Unavyotekeleza Mradi wa umeme Bwawa la nyerere Mama waonyeshe Oh, waonyeshe Unavyotekeleza Ikulu chamwino dodoma Izidi songa mbele Mama waonyeshe Oh, waonyeshe Unavyotekeleza