Mwanamke ni mtu na nusu Kukatishwa tamaa usiruhusu Mwanamke ni mtu na nusu Kurudishwa nyuma usiruhusu Na kam mwanaume ndio kichwa Cha familia Basi mwanamke ndio shingo Na kiwiliwili Amani ya mume alie bora Inatengenezwa na mke Anapoianza siku Hata furaha ya mume alie bora Inakamilishwa na mke Ifikapo usiku Si ujinga kukubali matokeo Na sio swala la kupinga Wanatuzidi upeo Ingekuwa hiari yangu mimi Ningewapa kila cheo Muadilifu kama mama yangu Sijamuona mpaka leo Samia Suluhu Ni mtu na nusu Mboni mpaye mpango Ni mtu na nusu Mariam mwinyi Ni mtu na nusu Marry Majaliwa Ni mtu na nusu Okt Tulia Ni mtu na nusu Anne Makinda Ni mtu na nusu Bibi Titi Ni mtu na nusu Sophia kawawa Ni mtu na nusu Patakucha litazama Hadi ifike kiama Huto muona kama mama mama Mwanamke ni kiumbe jasiri Mama ndie mungu wa pili Ile miezi tisa ni siri Baba asingeweza hata miwili Hata uwe tajiri, tajiri Kamwe huwezi kuwa na mama wawili, wawili Mume ataoa wawili, wawili Mwanamke hawezi kuwa na wawili Fikiri Sio ujinga kukubali matokeo Na sio swala la kupinga Wanatuzidi upeo Ingekuwa hiari yangu mimi Ningewapa kila cheo Muadilifu kama mama konde Sijamuona mpaka leo Maria Nyerere Ni mtu na nusu Bi Fatuma Karume Ni mtu na nusu Siti Mwinyi Ni mtu na nusu Mama Anna Mkapa Ni mtu na nusu Salma Kikwete Ni mtu na nusu Janet Magufuli Ni mtu na nusu Getrude Mongelia Ni mtu na nusu Bi Mwenda Ni mtu na nusu Bi Kidude Ni mtu na nusu Mama Khadija Kopa Ni mtu na nusu Yaw yaw Kondeboy call me number one Number one It's Konde music worldwide